HABARI NJEMA ZA NENO LA MUNGU.
HABARI NJEMA ZA NENO LA MUNGU.
MITHALI 15
3.Macho ya Bwana yako kila mahali;Yakimchunguza Mbaya na Mwema.
FUNDISHISHO.
Neno la Leo linatusisitiza kuwa Mwanadamu huwezi kumficha Mungu Jambo/Tendo Lolote.
Kama kuna jambo ambalo mwanadamu hujidanganya! Basi ni hili la kujificha wakati wa kutenda dhambi, akidhani kuwa kwasababu watu hawajamuona, basi hata Mungu hajawaona. Halafu utaona wanajifariji na kesho yake utamuona kanisani/hata kwenye Mikusanyiko ya Kidini,Akihudumu.
Huko ni kujidanganya sana.
Kama macho ya Mungu yako kila mahali yakimchunguza mwema na mbaya, wewe unamdanganya nani? Tambua jambo moja kuwa utamficha Mchungaji wako na washirika wenzako kanisani, lakini Mungu anakutambua vizuri tabia na mienendo yako kuwa ni michafu na haustahili katika ufalme wake.
Sasa hapo ujiulize ni jambo lipi utakalolifanya Mungu asilijue, kama anajua hadi mawazo yako unayoyawaza kabla ya kutenda jambo wenyewe?
Pia tambua kuwa hakuna jambo lililofichwa mbele za Mungu
Kwahiyo kwasababu hakuna jambo tunaloweza kulificha mbele za uso wa Mungu, hatuna budi kutenda yaliyo mema ili tuweze kuhesabiwa haki mbele zake.Kwa kutubu na kuziacha njia zetu mbaya zote.Maana Mungu watu ni mwenye huruma Atatusamehe kabisa wala hatakumbuka Muovu yetu ya Kwanza. Rejea. zaburi 139:1-4 1samweli 16:7 Waebrania 4:13
Mtakatifu Mtakatifu Bwana wa Majeshi Asante kwa kutulinda na hatari zote za usiku umetuwezesha kuiona tena siku hii mpya kwetu, wapo wenzetu wengi walitamani kuiona siku hii Lakini hawakuiona sio kwamba wao ni wenye dhambi kuliko sisi au sisi ni wenye haki kuliko wao ila ni kwa Neema Yako tu kwetu Mungu wetu.
Tunawaombea Wagonjwa mbalimbali waliopo katika Mahospatali Mbalimbali na wanaougulia Majumbani na sehemu mbalimbali wengine wapo safarini katika harakati za kutafuta Matibabu sahihi kwa Magonjwa yao,pia wapo ambao ni Wagonjwa Lakini bado hawajatambua kama ni Wagonjwa pamoja na wazee kwa umri wanaopitia Magonjwa na madhaifu mbalimbali kwasababu ya umri mkubwa Tunawaombea wote kila mmoja umguse na mkono wako wa Uponyaji na kuwaponya kabisa Magonjwa yao kwa kuwa Bwana Wewe ndiye Mponyaji pekee. Wapo miongoni mwetu wanaopitia Majaribu mbalimbali katika Maisha yao ya kila siku,Tunakuomba Bwana wetu waondolee yote hayo ikiwemo kutengwa na Jamii,kukosa Amani katika Mahusiano yao,Ndoa,Manyanyaso mbalimbali katika ajira zao pamoja na masengenyo pia wapo wanaokosa hata Mlo Moja kwa siku,Tunakuomba uwaondolee hayo yote ili nao waweze kufurahia Maisha yao uliyowapatia hapa Duniani.
Tunaomba yote haya tukiongozwa na Roho Mtakatifu kwa jina la Yesu Kristo Bwana na Mwokozi wetu. AMEEN
Gwakisa fk
05.06.2022
Comments
Post a Comment