Posts

VINYWA VYA MOYO: JINSI YA KULINDA MOYO WAKO-2

  Mithali 4;23  " Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo; Maana ndiko zitokako chemchemi za uzima” Karibu tuendelee kujifunza jinsi ya Kulinda Moyo, leo tunaendelea kwa Kuangalia Vinywa vya Moyo ambavyo kwa hivyo Moyo wa mtu Hula. Vinywa vya Moyo 1.                  Macho. Macho ni mdomo wa moyo, chochote kiingiacho kwa macho hicho huenda moja kwa moja kwenye moyo na hicho ndicho kiwezacho kuutia moyo Unajisi.Mtu anapokuwa anatazama kwa macho yake anakuwa anakula, yaani anamlisha mtu wa ndani (moyo wake).Yesu alisema mtu mwema kutoka kwenye akiba njema na mtu mwovu kutoka kwenye akiba mbovu, hapo juu nimekwambia kuwa Akiba hukaa ghalani na akiba haijii automatically kwenye ghala, bali huwekwa ghalani na ndipo baadae hutoka.   Tuangalie kwenye Mithali Jinsi akiba inavyotengenezwa ndani ya moyo na baadae itadhihirika.Weka ili moyoni kuwa kuna milango ambayo kwa hiyo kilichoko ...

LINDA SAANA MOYO WAKO KULIKO VYOTE ULINDAVYO: JINSI YA KULINDA MOYO WAKO-I

  Mithali 4;23 "Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo; Maana ndiko zitokako chemchemi za uzima" Bwana Yesu asifiwe,karibu tujifunze kwa pamoja kwa Roho wa Kweli jinsi ya kulinda moyo wako.Somo letu litakuwa likitoka katika kitabu cha Mithali 4;23 Ni Neno ambalo linaweza likawa sio mara yako ya kwanza kulisikia lakini embu fungua moyo wako ili Mungu akufundishe kwa undani juu ya Mstari huu,nami naamini baada ya kusoma hutabiki na ufahamu uliokuwa nawo kabla ya kusoma na mfumo wa maisha wako utaathiriwa na ufahamu ambao neno hili litauachilia ndani yako. Neno linasema Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo,maana huko ndiko zitokako chemichemi za Uzima" Kitu cha kwanza unachotakiwa kujua ni kuwa Unajukumu la kuulinda moyo wako,tena kuulinda kuliko yote ulindayo. Tuanze kwaa kujifunza Moyo ni nini hasa hata tukatakiwa kuulinda kuliko vyote tunavyolinda. Kwa lugha nyepesi Biblia inazungumzia Moyo kwa maana kama 4 hivi; a)Moyo ni chanzo/kiini cha Uhai wa kitu. b)Moyo ni kiun...

NGUVU ILIYO NDANI YA MWAMINIFU

MATENDO 2:1-4 "Hata ilipotimia siku ya Pentekoste walikuwako wote mahali pamoja. "Kukaja ghafula toka mbinguni uvumi kama uvumi wa upepo wa nguvu ukienda kasi,  ukaijaza nyumba yote waliyokuwa wameketi. "Kukawatokea ndimi zilizogawanyikana, kama ndimi za moto uliowakalia kila mmoja wao. "Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia kutamka." 💦Nguvu inapoingia ndani ya mwamini inaweka badiliko ndani yake Badiliko la milele lakini hilo badiliko linatunzwa na UTAKATIFU mana Roho Mtakatifu anaketi mahali pa Takatifu  💦Nguvu za Roho Mtakatifu zinatupa kumshinda shetani kwa namna yoyote ile  Shetani sio kwamba anatuogopa sisi ila anaogopa kile kilicho ndani yetu. 💦Pia huwezi kuona nguvu za Mungu kama unafanya mazoea kwenye kazi ya Mungu   Ondoka kwenye mazoea ili uone nguvu  na Baraka za Mungu .

OMBA MAOMBI YASIYOKOMA/ OMBENI BILA KUKOMA

Imeandikwa "ombeni bila kukoma; "1 Wathesalonike 5:17 Bwana Yesu asifiwe... Miujiza yetu sisi binadamu tulio chini ya jua hili,ipo katika maombi yasiyokoma.Mafanikio yetu yapo katika maombi yasiyokoma,Paulo mtume aliyetumwa na Mungu Baba na Yesu Kristo wala sio mwanadamu yeye anatuamsha siku ya leo akituambia TUOMBE BILA KUKOMA. Yesu naye ameweka msisitizo huo huo akituambia ; "Akawaambia mfano, ya kwamba imewapasa kumwomba Mungu sikuzote, wala wasikate tamaa. " Luka 18:1. Pale asemapo "Kumuomba Mungu sikuzote" maana yake ni kuomba pasipo kukoma. Mtu aombaye siku zote yaani bila kukoma,haimaanishi kwamba mtu huyo asikiwi na Mungu. Bali mtu wa namna hii ujiwekea akiba,na kuwa shupavu na shujaa wa kiroho. Tabia moja wapo ya Bwana wetu Yesu Kristo ni kuomba bila kukoma. Sisi tukiwa wanafunzi wake,basi hatuna budi kujifunza kwake. Leo nimekuandikia ujumbe huu kwa sababu najua shida kubwa ya wakristo wengi wa leo ni kwamba hawaombi au wanaomba lakini si...

YESU ANAKUPENDA SANA

Yohana 3: 16-17 “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. Maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye.” Mungu anakupenda sana, anajua jinsi unavyoenenda na amemtuma Mwana wake wa pekee, Yesu afe msalabani kwa ajili ya ukombozi wako. Haupaswi tena kuendelea kuishi dhambini, neema ya wokovu imefunuliwa na yapatikana bure kwa kumkiri na kumwamini Yesu. Warumi 10: 9-10 “Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako yakuwa ni BWANA, na kuamini moyoni mwako yakuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka. Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu.” Amua leo kumpa Yesu maisha yako upate tumaini jipya la uzima wa milele. Ukimpokea Yesu utapata furaha, amani na uzima wa kweli. Huwezi kuzipata baraka za Mungu kama hauna ushirika naye, na pia huwezi kushinda dhambi bila msaada wa Mungu. Kama upo tayari kum...

MAMBO YA KUEPUKA ILI KUTUNZA MISINGI YA IMANI KABLA YA KUANZISHA MAHUSIANO YA UCHUMBA HADI NDOA

. 1. Epuka kuanzisha mahusiano na mtu asiye amini. Ijue kwanza imani ya mtu kabla ya kuanza naye mahusiano ya uchumba.  Malaki 2:10 - 11 Malaki 2:10-11 [10]Je! Sisi sote hatuna Baba mmoja? Mungu aliyetuumba siye mmoja tu? Basi, mbona kila mmoja wetu anamtenda ndugu yake mambo ya hiana, tukilinajisi agano la baba zetu? [11]Yuda ametenda kwa hiana, na chukizo limetendeka katika Israeli, na katika Yerusalemu; maana Yuda ameunajisi utakatifu wa BWANA aupendao,  naye amemwoa binti ya mungu mgeni. ​ 2. Epuka kuanzisha mahusiano kwa kufuata namna, au kawaida au desturi ya dunia hii au ulimwengu huu. Dunia wana mungu wao na sisi tulioamini tuna Mungu wetu kwa hiyo kawaida, namna na desturi zetu zinapingana na zao. Walawi 18:30 [ 30]Kwa ajili ya hayo yashikeni mausia yangu, ili kwamba  msifanye kabisa desturi hizi  zichukizazo mojawapo, zilizotangulia kufanywa mbele zenu, wala msijitie unajisi katika mambo hayo; mimi ndimi BWANA, Mungu wenu. ​ Walawi 20:23 [23]Nanyi msiende k...

Hii ndio sababu kwanini utaoa/olewa na mtu asiye sahihi

Image
Wangapi wanaweza kukiri kuwa wanahisi wameoa/wameolewa na mtu asiye sahihi? Basi mimi nipo hapa kutoa ushauri nasaha pamoja na faraja kwenu. Unajua watu wengi tuna hasira tulizozibeba ndani yetu juu ya mahusiano yetu ya kimapenzi, jinsi mahusiano yetu yalivyoenda. Leo kazi yangu ni kugeuza hasira hiyo kuwa huzuni. Ukiweza kugeuza hasira kuwa majonzi, unakuwa umepiga hatua kisaikolojia. Mara nyingi huwa tunafikiri mtu mwenye hasira ni mtu flani muovu, au mtu mwenye kukata tamaa kirahisi. Si kweli!! Ukichunguza vizuri utagundua kuwa ndani ya mtu ambaye hukasirika mara kwa mara, kuna mtu flani mwenye matumaini makubwa! Yaani matumaini huzaa hasira! Fikiria mtu ambaye hupiga kelele kila akitafuta funguo zake, au akiwa amekwama kwenye foleni barabarani. Mtu huyo huonyesha kuwa na Imani (ingawa ya kizembe) ya dunia ambayo funguo huwa hazipotei na barabara ziko wazi tu muda wote. Kwahiyo ili tupunguze hasira tuliyonayo juu ya mahusiano yetu inabidi tupunguze baadhi ya matum...