OMBA MAOMBI YASIYOKOMA/ OMBENI BILA KUKOMA
Imeandikwa "ombeni bila kukoma; "1 Wathesalonike 5:17 Bwana Yesu
asifiwe... Miujiza yetu sisi binadamu tulio chini ya jua hili,ipo katika maombi
yasiyokoma.Mafanikio yetu yapo katika maombi yasiyokoma,Paulo mtume aliyetumwa
na Mungu Baba na Yesu Kristo wala sio mwanadamu yeye anatuamsha siku ya leo
akituambia TUOMBE BILA KUKOMA. Yesu naye ameweka msisitizo huo huo akituambia ;
"Akawaambia mfano, ya kwamba imewapasa kumwomba Mungu sikuzote, wala
wasikate tamaa. " Luka 18:1.
Pale asemapo "Kumuomba Mungu sikuzote" maana yake ni kuomba pasipo
kukoma. Mtu aombaye siku zote yaani bila kukoma,haimaanishi kwamba mtu huyo
asikiwi na Mungu. Bali mtu wa namna hii ujiwekea akiba,na kuwa shupavu na
shujaa wa kiroho.
Tabia moja wapo ya Bwana wetu Yesu Kristo ni kuomba bila
kukoma. Sisi tukiwa wanafunzi wake,basi hatuna budi kujifunza kwake. Leo
nimekuandikia ujumbe huu kwa sababu najua shida kubwa ya wakristo wengi wa leo
ni kwamba hawaombi au wanaomba lakini sio maombi ya pasipo kukoma,zaidi sana
kuombewa tu. Ifike wakati sasa,uanze kuomba wewe mwenyewe bila kukoma hata kama
unaombewa maana kuombewa si vibaya. Wakristo wa leo tuna maneno mengi sana,bali
kuomba ni kwa muda mfupi sana tena wakati mwingine ni kwa kupapasa papasa.Ikiwa
kama hali itakuwa hivyo basi tutaonewa na mapepo.
● Maombi huenda sambamba na neno la Kristo. Maana pasipo kuwa na neno
hutashindwa kujua mafunuo ya jinsi gani ya kuomba. Zipo silaha nyingi dhidi ya
adui katika ulimwengu wa roho kwetu sisi wakristo. Maombi yasiyokoma ni silaha
kubwa isiyoelezeka. Ipo mafano mingi katika Biblia takatifu,yenye kutuonesha
majibu ya maombi ya kungangana(Maombi bila kukoma) Mfano;
Tumwangalie Danieli, Imeandikwa;
Basi mfalme akatoa amri, nao wakamleta Danielii, wakamtupa
katika tundu la simba. Mfalme akanena, akamwambia Danielii, Mungu wako
unayemtumikia daima, yeye atakuponya. " Daniel 6:16 Danieli alikuwa
akimtumikia Mungu wake DAIMA. Kudumu katika maombi ni njia mojawapo ya
kutumikia ufalme wa Mungu. Danieli alikuwa akiomba kwa siku mara tatu.( Danieli
6:13). Hivyo mtu huyu aliomba bila kukoma. Kiwango chako cha maombi hakitoshi.
Yakupasa uongeze kiwango chako cha maombi. Kumbuka kadri unapozidi kuomba
ndivyo kadri unavyozidi kukaribia ushindi wako.
Yapo mambo mengine hayawezekani pasipo kuomba kwa kungangana. Maana si kila
jambo hutoka kwa maombi ya kawaida,mengine ni kwa kuomba bila kukoma. Neno la
leo linasisitiza kukaza katika kuomba pasipo kunyamaza,pasipo kuangalia umeomba
siku ngapi,au umeomba miezi mingapi,au umeomba miaka mingapi BALI KUOMBA PASIPO
KUKOMA! Nalipenda kanisa la kwanza ile namna walipomuombea Petro bila kukoma
pale Petro alipokuwa gerezani ( Matendo 12:1-15) Kanisa hili liliomba pasipo
kukomba mpaka majibu yalipopatikana. •Siku zote shetani huleta uchovu kwa yule
aombaye. Yaani unaweza kupanga kwamba unaanza kuomba,lakini unatashangaa uchovu
huja kwa gafula,au utashangaa mgeni huja akikuhitaji wewe uliyepanga kuomba,hizo
zote ni hila za adui.
Ukiona unavamiwa na hali kama hiyo,basi wewe usikome ukanyamaza hapo msii Roho
mtakatifu akupe muongozo. Kuomba bila kukoma ni kazi yako,kazi hii hakupewa
mwingine aweye yote bali umepewa wewe ndio maana hata ni wewe ambaye umeokoka
katika familia. Yoyote aliyeokoka uhesabiwa ni mlinzi au askari. Askari yeyote
yule ni lazima awe na silaha ili uaskari wake ukamilike,silaha yake yeye askari
wa kiroho ni maombi pasipo kukoma na neno la Kristo zaidi sana utauwa. Maombi
ili yanoge na yawe maombi haswaa Roho mtakatifu huhitajika sana. Kwa lugha
nyepesi Roho mtakatifu ndio msaidizi wetu,pasipo Yeye hakuna maombi yanayoweza
kufanywa. Ndugu,
Ukitaka kuona mpenyo wako,huna budi kuomba bila kukoma. Ukitaka magonjwa yasiwe
sehemu yako,huna budi kuomba bila kukoma, Ukitaka upako mara dufu,basi huna
budi kuomba bila kukoma, Ukitaka kufunguliwa katika vifungo sugu,huna budi
kuomba bila kukoma.
Comments
Post a Comment