NGUVU ILIYO NDANI YA MWAMINIFU
MATENDO 2:1-4
"Hata ilipotimia siku ya Pentekoste walikuwako wote mahali pamoja.
"Kukaja ghafula toka mbinguni uvumi kama uvumi wa upepo wa nguvu ukienda kasi,
ukaijaza nyumba yote waliyokuwa wameketi.
"Kukawatokea ndimi zilizogawanyikana, kama ndimi za moto uliowakalia kila mmoja wao.
"Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia kutamka."
💦Nguvu inapoingia ndani ya mwamini inaweka badiliko ndani yake
Badiliko la milele lakini hilo badiliko linatunzwa na UTAKATIFU mana Roho Mtakatifu anaketi mahali pa Takatifu
💦Nguvu za Roho Mtakatifu zinatupa kumshinda shetani kwa namna yoyote ile
Shetani sio kwamba anatuogopa sisi ila anaogopa kile kilicho ndani yetu.
💦Pia huwezi kuona nguvu za Mungu kama unafanya mazoea kwenye kazi ya Mungu
Ondoka kwenye mazoea ili uone nguvu na Baraka za Mungu .
Comments
Post a Comment