HAKI ZA WATOTO KATIKA KUMJUA MUNGU

 Kumbukumbu la Torati 6:7nawe uwafundishe watoto wako kwa bidii, na kuyanena uketipo katika nyumba yako, na utembeapo njiani, na ulalapo, na uondokapo.

WAZAZI NA JAMII wanatakiwa kutambua umuhimu wa kuwalinda watoto na kufahamu haki zao za msingi huku wakitambua kuwa swala la kuwalinda  watoto ni la kwetu sote badala ya kuwaachia serikali na mashirika binafsi. Zaburi 34:11 Njoni, enyi wana, mnisikilize, Nami nitawafundisha kumcha Bwana. Mithali 8:32-33 Basi, wanangu, nisikilizeni sasa; Maana heri hao wazishikao amri zangu. Sikieni mafundisho, mpate hekima, Wala msiikatae.

Jamii inayowazunguka watoto hawa ndio inayopaswa kuhakikisha inawalinda na matukio mbalimbali ya unyanyasaji yanayofanya kwenye jamii zao ikiwa ni pamoja na kuhakikisha mtoto anapewa nafasi ya kushiriki kikamilifu badala ya kunyanyapaliwa. Zaburi144:12 Wana wetu na wawe kama miche Waliokua ujanani. Binti zetu kama nguzo za pembeni Zilizonakishwa kwa kupamba hekalu.

 

Umefika wakati sasa wa jamii kuchukua hatua na kuanza kutokomeza matukio mbalimbali ya unyanyasaji  wanayofanyiwa watoto na kujikuta wengi wao wakiishia mitaani na hata wengine kujiunga na makundi mbalimbali yanayowapotosha. 1 Mambo ya Nyakati 17:8 nami nimekuwa pamoja nawe kila ulikokwenda, na kuwakatilia mbali adui zako wote mbele yako; nami nitakufanyia jina, kama jina la hao wakuu walioko duniani.

 

Jamii inapaswa kutambua kuwa ina wajibu mkubwa sana wa kumlinda mtoto yoyote aliyeko katika jamii kwa kumpatia haki zake za msingi badala ya kutegemea mashirika mbalimbali na serikali kufanya mambo hayo. Theluthi mbili ya watoto wanaamini kwamba wazazi au watu wazima wana uwezo wa kuondoa haki za watoto na nusu ya watoto wanasema kuwa wazazi ndio wanaoamua  ni haki zipi ambazo watoto wanapaswa kuwa nazo. Zaburi 21:7-9 Kwa kuwa mfalme humtumaini Bwana, Na kwa fadhili zake Aliye juu hataondoshwa. Mkono wako utawapata adui zako wote, Mkono wako wa kuume utawapata wanaokuchukia. Utawafanya kuwa kama tanuru ya moto, Wakati wa ghadhabu yako. Bwana atawameza kwa ghadhabu yake, Na moto utawala.

 

Watoto wengi wanahitaji haki zao za msingi kama vile kupata elimu, mavazi,malazi, chakula na ulinzi na endapo watapatiwa haki zao  itawasaidia kwa kiasi kikubwa sana kutulia na hatimaye kujidhamini wao wenyewe. Wazazi na jamii  kwa ujumla wanatakiwa kupewa ushauri juu ya umuhimu wa kumjali mtoto na kumpatia haki zake za msingi ikiwa ni pamoja na kumlinda juu ya matukio mbalimbali ya unyanyasaji .

Wewe kama mzazi au mzazi mtarajiwa anza kufanya mazoezi ya kuwapatia watoto wako haki zao za msingi au jiandae kuwapatia watoto haki zao, ukisikia kuna semina mahali ya kumhusu mtoto  nenda kasikilise ili upate elimu zaidi. 3Yohana 1:4 Sina furaha iliyo kuu kuliko hii, kusikia ya kwamba watoto wangu wanakwenda katika kweli.
Wapendwa wengi sana tumezoea kusema kwamba (Na watoto wako wote watafundishwa na Bwana; na amani ya watoto wako itakuwa nyingi. Isaya54:13) Sipingi kwamba watafundishwa na Bwana ila kumbuka Mungu amekupa hao watoto umtunzie na wakiharibika utadaiwa kwa nini hukuwafundisha katika njia ipasavyo ili waweza kumpendeza Mungu. Mithali 22:6 Mlee mtoto katika njia impasayo, Naye hataiacha, hata atakapokuwa mzee
Yohana 21:15 Basi walipokwisha kula, Yesu akamwambia Simoni Petro, Je! Simoni wa Yohana, wewe wanipenda kuliko hawa? Akamwambia , Naam ,Bwana, wewe wajua kuwa nakupenda. Akamwambia, Lisha wana-kondoo wangu.
Mithali 4: 4,5 Naye akanifundisha, akaniambia, Moyo wako uyahifadhi maneno yangu; Shika amri zangu ukaishi. Jipatie hekima, jipatie ufahamu; usiusahau; Wala usiyakatae maneno ya kinywa changu.
Mungu wa Mbinguni atusaidie HEKIMA na maarifa mengi ili tuweze kuwalea watoto jinsi atakavyo yeye ili waweze kumpendeza yeye.



Comments

Popular posts from this blog

LINDA SAANA MOYO WAKO KULIKO VYOTE ULINDAVYO: JINSI YA KULINDA MOYO WAKO-I

VINYWA VYA MOYO: JINSI YA KULINDA MOYO WAKO-2

Ufanye Nini Unapoumizwa Moyo Na Watu Wako Wa Karibu/ Jinsi Ya Kupokea Uponyaji kwa Moyo Ulioumizwa