HAKI ZA WATOTO
Kumbukumbu la Torati 6:7nawe uwafundishe watoto wako kwa
bidii, na kuyanena uketipo katika nyumba yako, na utembeapo njiani, na ulalapo,
na uondokapo.
WAZAZI NA JAMII wanatakiwa kutambua umuhimu wa kuwalinda
watoto na kufahamu haki zao za msingi huku wakitambua kuwa swala la kuwalinda
watoto ni la kwetu sote badala ya kuwaachia serikali na mashirika
binafsi. Zaburi 34:11 Njoni, enyi wana, mnisikilize, Nami
nitawafundisha kumcha Bwana. Mithali 8:32-33 Basi, wanangu,
nisikilizeni sasa; Maana heri hao wazishikao amri zangu. Sikieni mafundisho,
mpate hekima, Wala msiikatae.
Jamii inayowazunguka watoto hawa ndio inayopaswa kuhakikisha
inawalinda na matukio mbalimbali ya unyanyasaji yanayofanya kwenye jamii zao
ikiwa ni pamoja na kuhakikisha mtoto anapewa nafasi ya kushiriki kikamilifu
badala ya kunyanyapaliwa. Zaburi144:12 Wana wetu na wawe kama miche
Waliokua ujanani. Binti zetu kama nguzo za pembeni Zilizonakishwa kwa kupamba
hekalu.
Umefika wakati sasa wa jamii kuchukua hatua na kuanza
kutokomeza matukio mbalimbali ya unyanyasaji wanayofanyiwa watoto na
kujikuta wengi wao wakiishia mitaani na hata wengine kujiunga na makundi
mbalimbali yanayowapotosha. 1 Mambo ya Nyakati 17:8 nami nimekuwa
pamoja nawe kila ulikokwenda, na kuwakatilia mbali adui zako wote mbele yako;
nami nitakufanyia jina, kama jina la hao wakuu walioko duniani.
Jamii inapaswa kutambua kuwa ina wajibu mkubwa sana wa
kumlinda mtoto yoyote aliyeko katika jamii kwa kumpatia haki zake za msingi
badala ya kutegemea mashirika mbalimbali na serikali kufanya mambo
hayo. Theluthi mbili ya watoto wanaamini kwamba wazazi au watu wazima wana
uwezo wa kuondoa haki za watoto na nusu ya watoto wanasema kuwa wazazi ndio
wanaoamua ni haki zipi ambazo watoto wanapaswa kuwa nazo. Zaburi
21:7-9 Kwa kuwa mfalme humtumaini Bwana, Na kwa fadhili zake Aliye juu
hataondoshwa. Mkono wako utawapata adui zako wote, Mkono wako wa kuume
utawapata wanaokuchukia. Utawafanya kuwa kama tanuru ya moto, Wakati wa
ghadhabu yako. Bwana atawameza kwa ghadhabu yake, Na moto utawala.
Watoto wengi wanahitaji haki zao za msingi kama vile kupata
elimu, mavazi,malazi, chakula na ulinzi na endapo watapatiwa haki zao
itawasaidia kwa kiasi kikubwa sana kutulia na hatimaye kujidhamini wao
wenyewe. Wazazi na jamii kwa ujumla wanatakiwa kupewa
ushauri juu ya umuhimu wa kumjali mtoto na kumpatia haki zake za msingi ikiwa
ni pamoja na kumlinda juu ya matukio mbalimbali ya unyanyasaji .
Wewe kama mzazi au mzazi mtarajiwa anza kufanya mazoezi ya
kuwapatia watoto wako haki zao za msingi au jiandae kuwapatia watoto haki zao,
ukisikia kuna semina mahali ya kumhusu mtoto nenda kasikilise ili
upate elimu zaidi. 3Yohana 1:4 Sina furaha iliyo kuu kuliko hii,
kusikia ya kwamba watoto wangu wanakwenda katika kweli.
Wapendwa wengi sana tumezoea kusema kwamba (Na watoto wako wote watafundishwa
na Bwana; na amani ya watoto wako itakuwa nyingi. Isaya54:13) Sipingi
kwamba watafundishwa na Bwana ila kumbuka Mungu amekupa hao watoto umtunzie na
wakiharibika utadaiwa kwa nini hukuwafundisha katika njia ipasavyo ili waweza
kumpendeza Mungu. Mithali 22:6 Mlee mtoto katika njia impasayo, Naye
hataiacha, hata atakapokuwa mzee
Yohana 21:15 Basi walipokwisha kula, Yesu akamwambia Simoni Petro, Je!
Simoni wa Yohana, wewe wanipenda kuliko hawa? Akamwambia , Naam ,Bwana, wewe
wajua kuwa nakupenda. Akamwambia, Lisha wana-kondoo wangu.
Mithali 4: 4,5 Naye akanifundisha, akaniambia, Moyo wako uyahifadhi maneno
yangu; Shika amri zangu ukaishi. Jipatie hekima, jipatie ufahamu; usiusahau;
Wala usiyakatae maneno ya kinywa changu.
Mungu wa Mbinguni atusaidie HEKIMA na maarifa mengi ili tuweze kuwalea watoto
jinsi atakavyo yeye ili waweze kumpendeza yeye.
Comments
Post a Comment