Jinsi kutumia Muda Wako Vizuri
Wakolosai 4:5 Waefeso 5:14-16
Maana ya Muda
Muda ni mali yenye dhamani kama ilivyo pesa yako, nyumba
yako, gari lako, kitanda chako nk
Ndio maana wazungu wanasema “Time is Money”
Hautengenezwi na mtu, ni Mungu mwenyewe ametupa
kwa hiyo ni busara kuutumia vizuri
Haufugiki ukipotea umepotea, haurudi
“Opportunities comes and go, they will never come back”
“Fursa huja na kwenda, hazirudi tena”
If you love life, don't waste time, for time is what life
is made up of. Bruce Lee
Wakati ni ukuta (ina mwisho)
“Time the time before it times you”
Lost time is never found again. Benjamin
Franklin
“Time is what we want most, but what we use
worst.” ― William Penn
“You may delay, but time will not.”
― Benjamin Franklin
Tunatumia muda vizuri kwa sababu nyakati hizi ni za uovu
Usipoutumia muda vizuri, utautumia vibaya kwa kufanya maovu
-Waefeso 5:16
a. Kukua kiroho
b. Kupata maendeleo ya
kielimu, kiuchumi, nk
c. Kuheshimika
katika jamii
d. Kutengeneza mahusiano
mazuri na wenzako
e. Kudumaa kiroho
f. Kurudi
nyuma kimaendeleo kama ya kielimu, kiuchumi, nk
g. Kukosa heshima
katika jamii
h. Kuharibu mahusiano
mazuri na wenzako
Hatua za Jinsi
ya Kutumia Muda Wako Vizuri
1. Kumtanguliza/Kumtegemea
Yesu
Kumtanguliza/Kumtegemea Yesu Katika Muda/Ratiba Yako Waefeso
5:14
2. Kutathmini
jinsi ulivyotumia muda huko nyuma
Kutafakari na kutathmini jinsi ulivyotumia muda huko
nyuma Waefeso – 5:15
a. Weka ratiba yako
ya zamani ikiwa na vitu/shughuli muhimu kama kazi zako za kawaida, shughuli za
kiroho kama maombi, kuhubiri, kushuhudia nk, shughuli za kanisani
b. Weka maksi kwa
kukadiria ni shughuli ngapi umeweza kutimiza kwa ufanisi upi na zipi
hukufanikiwa
c. Eleza pia nguvu
na fursa zilizokuwezesha kufanikiwa na udhaifu pamoja na pingamizi
zilizosababisha ushindwe kutimiza
|
Tarehe |
Kazi/Shughuli |
Kiwango
cha ufanisi ktk % |
Sababu
za ufanisi au za kushindwa |
2. Kubuni na
kupanga ratiba kwa kuzingatia tathmini hapo juu Waefeso 5:16, Wakolasai
|
Tarehe |
Kazi/Shughuli |
Kiwango
cha ufanisi |
Kuweka vipaumbele katika kuitekeleza ratiba yako Waefeso
5:16, Wakolasai 4:5,
Jedwali la shughuli za kila siku
|
|
HARAKA |
SIO
HARAKA |
|
MUHIMU |
I -
Matatizo Msongo wa
Matatizo |
II - Kazi za
Maendeleo Kufanya
mambo katika mpangilio mzuri |
|
SIO
MUHIMU |
III
– Dharura Kuendeshwa
na mambo ya watu wengine |
IV -
Vipoteza Muda Kufanya
mambo yasiyo kwenye ratiba |
Jedwali linaloonyesha aina ya shughuli na vipaumbele
|
HARAKA |
SIO
HARAKA |
|
|
MUHIMU |
I -
Matatizo Msongo wa
Matatizo § Kifo,
mafuriko, magonjwa n.k. Kazi
zote muhimu na haraka lakini ni nje ya ratiba. Ratiba: Huongozwa na matatizo Matokeo
ni: Kukosa maendeleo ya kimwili na kiroho. Kwa sababu ya kufanya mambo
kwa kiti moto, mahangaiko tu na kuchanganyikiwa |
II -
Kazi za Maendeleo Kufanya
mambo katika mpangilio mzuri § Kujenga
nyumba § Kulima
shamba § Kusoma na
kusomesha § Kuhudhururia
ibada nk Kazi
zote ambazo sio za haraka lakini ni za kupangwa. Ratiba:
Huongozwa na mpangaji wa ratiba Matokeo
ni: Kupata maendeleo ya kimwili na kiroho kwa sababu
ya Nidhamu na Mpango Mzuri wa kazi nk |
|
SIO
MUHIMU |
III
- Dharura Kuendeshwa
na mambo ya watu wengine Simu, barua, mgeni, harusi, mialiko n.k. Kazi
zote zinazoingilia ratiba ambazo sio muhimu lakini ni za haraka. Ratiba:
Huongozwa na watu wengine Matokeo
ni: Kukosa maendeleo kwa sababu ya Kupelekeshwa na wengine, kufanya
kazi katika woga, hakuna kuona mbali hapa |
IV -
Vipoteza Muda Kufanya
mambo yasiyo kwenye ratiba Karata, Bao, Kutembelea
wengine, Kuangalia
TV, Radio, Video, Facebook, n.k. Vitu
vyote vya kupoteza muda sio
muhimu, sio haraka. Ratiba:
Hakuna ratiba kwa sababu ya ambo yasiyopangwa Matokeo
ni: Umaskini, kurudi nyuma kiroho, Kutowajibika kwa ujumla,
kufukuzwa kazini, kuwa mzigo kwa ndugu au rafiki Kumb:
Asiyefanya kazi na asile 2Thel 3:10,11 |
Kuomba Hekima Katika Kusimami na Kutekeleza Ratiba na Mambo
nje ya Ratiba (mambo ya dharura hasa yale ya kiboksi cha kwanza) Waefeso 1: 17,
Yakobo 1.5
Jizoeze kutoahirisha jambo/mambo/shughuli
6. Kufanya
mambo zaidi ya moja kwa wakati mmoja
Jizoeze kufanya mambo zaidi ya moja kwa wakati mmoja kwa
yale mambo yanayowezekana
7. Kuweka
kumbumbuku ya namna ya kufanya jambo
Kuweka kumbumbuku ya namna ya kufanya jambo kwa urahisi na
ufanisi zaidi ili ikusaidie kwenye utendaji wa huko mbeleni kwa kuboresha zaidi
Katika kuhitimisha ni vizuri kujua na kuukubali ukweli kuwa
matumizi ya muda ni ya tabia na utamaduni zaidi. Hivyo hauwezi kuwa jana tu
unatumia muda vibaya na leo ukageuka na kuwa unatumia muda vizuri.
Ili uweze kubadili tabia na utamaduni wako wa kutumia muda
vibaya kwenda kwenye maadili ya kutumia muda vizuri ni vyema yafuatayo yatokee
kwako:
1. Kukubali ukweli
na kukubali kugeuka kwa kubadilika kifikra
2. Kumtanguliza
Mungu katika yote
3. Kukubali pia
kujifunza namna ya kuutumia muda vizuri kutoka katika maandiko na walimu au
marafiki zako
4. Kuchukua hatua
ya kujizoeza kuutumia muda vizuri kwa kufanya kidogokidogo
5. Kijitathmini
kila baada ya muda Fulani (hapa unaweza kuwatumia watu wengine)
6. Fundisha la
elekeza haya kwa watoto wako
Mungu akubariki na kukuwezesha kuutumia muda vizuri
Comments
Post a Comment