Jinsi kutumia Muda Wako Vizuri
Wakolosai 4:5 Waefeso 5:14-16
Maana ya Muda
Muda ni mali yenye dhamani kama ilivyo pesa yako, nyumba yako, gari lako, kitanda chako nk
Ndio maana wazungu wanasema “Time is Money”
Sifa za Muda
Hautengenezwi
Hautengenezwi na mtu, ni Mungu mwenyewe ametupa kwa hiyo ni busara kuutumia vizuri
Haufugiki
Haufugiki ukipotea umepotea, haurudi
“Opportunities comes and go, they will never come back”
“Fursa huja na kwenda, hazirudi tena”
Muda ni maisha
Hausubiri,
Wakati ni ukuta (ina mwisho)
“Time the time before it times you”
“Time is what we want most, but what we use worst.” ― William Penn
“You may delay, but time will not.”
― Benjamin Franklin
― Benjamin Franklin
Kwa nini kutumia muda vizuri?
Tunatumia muda vizuri kwa sababu nyakati hizi ni za uovu
Usipoutumia muda vizuri, utautumia vibaya kwa kufanya maovu -Waefeso 5:16
Faida za kutumia muda vizuri
a. Kukua kiroho
b. Kupata maendeleo ya kielimu, kiuchumi, nk
c. Kuheshimika katika jamii
d. Kutengeneza mahusiano mazuri na wenzako
Hasara za kutumia muda vibaya
e. Kudumaa kiroho
f. Kurudi nyuma kimaendeleo kama ya kielimu, kiuchumi, nk
g. Kukosa heshima katika jamii
h. Kuharibu mahusiano mazuri na wenzakoHatua za Jinsi ya Kutumia Muda Wako Vizuri
1. Kumtanguliza/Kumtegemea Yesu
Kumtanguliza/Kumtegemea Yesu Katika Muda/Ratiba Yako Waefeso 5:14
2. Kutathmini jinsi ulivyotumia muda huko nyuma
Kutafakari na kutathmini jinsi ulivyotumia muda huko nyuma Waefeso – 5:15
a. Weka ratiba yako ya zamani ikiwa na vitu/shughuli muhimu kama kazi zako za kawaida, shughuli za kiroho kama maombi, kuhubiri, kushuhudia nk, shughuli za kanisani
b. Weka maksi kwa kukadiria ni shughuli ngapi umeweza kutimiza kwa ufanisi upi na zipi hukufanikiwa
c. Eleza pia nguvu na fursa zilizokuwezesha kufanikiwa na udhaifu pamoja na pingamizi zilizosababisha ushindwe kutimiza
Mfano wa ratiba ya tadhimini
Tarehe | Kazi/Shughuli | Kiwango cha ufanisi ktk % | Sababu za ufanisi au za kushindwa |
2. Kubuni na kupanga ratiba kwa kuzingatia tathmini hapo juu Waefeso 5:16, Wakolasai
Mfano wa ratiba ya maboresho
Tarehe | Kazi/Shughuli | Kiwango cha ufanisi |
3. Kuweka vipaumbele
Kuweka vipaumbele katika kuitekeleza ratiba yako Waefeso 5:16, Wakolasai 4:5,
Jedwali la shughuli za kila siku
HARAKA | SIO HARAKA | |
MUHIMU | I - Matatizo Msongo wa Matatizo | II - Kazi za Maendeleo Kufanya mambo katika mpangilio mzuri |
SIO MUHIMU | III – Dharura Kuendeshwa na mambo ya watu wengine | IV - Vipoteza Muda Kufanya mambo yasiyo kwenye ratiba |
Jedwali linaloonyesha aina ya shughuli na vipaumbele
HARAKA | SIO HARAKA | |
MUHIMU | I - Matatizo Msongo wa Matatizo § Kifo, mafuriko, magonjwa n.k. Kazi zote muhimu na haraka lakini ni nje ya ratiba. Ratiba: Huongozwa na matatizo Matokeo ni: Kukosa maendeleo ya kimwili na kiroho. Kwa sababu ya kufanya mambo kwa kiti moto, mahangaiko tu na kuchanganyikiwa | II - Kazi za Maendeleo Kufanya mambo katika mpangilio mzuri § Kujenga nyumba § Kulima shamba § Kusoma na kusomesha § Kuhudhururia ibada nk Kazi zote ambazo sio za haraka lakini ni za kupangwa. Ratiba: Huongozwa na mpangaji wa ratiba Matokeo ni: Kupata maendeleo ya kimwili na kiroho kwa sababu ya Nidhamu na Mpango Mzuri wa kazi nk |
SIO MUHIMU | III - Dharura Kuendeshwa na mambo ya watu wengine Simu, barua, mgeni, harusi, mialiko n.k. Kazi zote zinazoingilia ratiba ambazo sio muhimu lakini ni za haraka. Ratiba: Huongozwa na watu wengine Matokeo ni: Kukosa maendeleo kwa sababu ya Kupelekeshwa na wengine, kufanya kazi katika woga, hakuna kuona mbali hapa | IV - Vipoteza Muda Kufanya mambo yasiyo kwenye ratiba Karata, Bao, Kutembelea wengine, Kuangalia TV, Radio, Video, Facebook, n.k. Vitu vyote vya kupoteza muda sio muhimu, sio haraka. Ratiba: Hakuna ratiba kwa sababu ya ambo yasiyopangwa Matokeo ni: Umaskini, kurudi nyuma kiroho, Kutowajibika kwa ujumla, kufukuzwa kazini, kuwa mzigo kwa ndugu au rafiki Kumb: Asiyefanya kazi na asile 2Thel 3:10,11 |
4. Kuomba Hekima
Kuomba Hekima Katika Kusimami na Kutekeleza Ratiba na Mambo nje ya Ratiba (mambo ya dharura hasa yale ya kiboksi cha kwanza) Waefeso 1: 17, Yakobo 1.5
5. Kutoahirisha jambo
Jizoeze kutoahirisha jambo/mambo/shughuli
6. Kufanya mambo zaidi ya moja kwa wakati mmoja
Jizoeze kufanya mambo zaidi ya moja kwa wakati mmoja kwa yale mambo yanayowezekana
7. Kuweka kumbumbuku ya namna ya kufanya jambo
Kuweka kumbumbuku ya namna ya kufanya jambo kwa urahisi na ufanisi zaidi ili ikusaidie kwenye utendaji wa huko mbeleni kwa kuboresha zaidi
Hitimisho
Katika kuhitimisha ni vizuri kujua na kuukubali ukweli kuwa matumizi ya muda ni ya tabia na utamaduni zaidi. Hivyo hauwezi kuwa jana tu unatumia muda vibaya na leo ukageuka na kuwa unatumia muda vizuri.
Ili uweze kubadili tabia na utamaduni wako wa kutumia muda vibaya kwenda kwenye maadili ya kutumia muda vizuri ni vyema yafuatayo yatokee kwako:
1. Kukubali ukweli na kukubali kugeuka kwa kubadilika kifikra
2. Kumtanguliza Mungu katika yote
3. Kukubali pia kujifunza namna ya kuutumia muda vizuri kutoka katika maandiko na walimu au marafiki zako
4. Kuchukua hatua ya kujizoeza kuutumia muda vizuri kwa kufanya kidogokidogo
5. Kijitathmini kila baada ya muda Fulani (hapa unaweza kuwatumia watu wengine)
6. Fundisha la elekeza haya kwa watoto wako
Mungu akubariki na kukuwezesha kuutumia muda vizuri
Comments
Post a Comment