Jinsi Ya Kushinda Kukata Tamaa

 



Sifuatazo ni baadhi ya hatua unazoweza kuchukua baada ya kujiona kuwa unaelekea kukata tamaa kutokana na hali ya maisha uliyonayo na pia mapito unayopitia. Kama mwana wa Mungu sikuzote hutakiwi kukata tamaa maana unapofanya hivyo unampa shetani nafasi kukukandamiza zaidi na hata pia kukuangusha.
1.      Watambue Wababe Walioko Langoni
Wababe wawili wanaolinda lango la kuingilia kwenye nchi ya ahadi hata leo wanaitwa hofu na kukata tamaa. Ikiwa sasa unasikia sauti zao, na kuhisi msukumo wa ushawishi wao, basi ujue kwamba upo karibu sana na ahadi zako. Katika kipindi hiki muhimu, kama ilivyokuwa kwa Yoshua, unapaswa kuwa hodari na moyo wa ushujaa na kusonga mbele katika neema anayokupa Mungu (Yos 1:9).
2.      Elewa Kinachoendelea
Katika 2Kor 4:16,17 Paulo anasema tusilegee kwa sababu kwa kupitia dhiki yetu utu wetu wa ndani unafanywa upya. Anasema dhiki yetu nyepesi na iliyo ya muda mfupi tu, inatufanyia kitu chema katika Mungu.
3.      Tumaini Kwa Mungu
Hata kama imani yako ni ndogo, bado unaweza kumtumaini Mungu na kuamini kwamba Mungu wa amani atamseta Shetani mara chini ya miguu yako (Zab 42:5) (Rum 16:20).
4.      Kiri Hitaji Lako, Mshirikishe Mwenzako Kisha Mwombe
Katika Mhu 4:12 tunaona kwamba uwezo wa watu wawili ni mkubwa kuliko wa mtu mmoja. Usihifadhi tu mawazo yako, mshirikishe mwenzako na halafu mwombe pamoja, na kumfunga Shetani.
5.      Pokea Kutoka Kwa Mungu
Fungua moyo wako na umwachie Roho Mtakatifu akuhudumie kwa habari ya saburi na faraja ya Mungu, tumaini, furaha na amani (Rum 15:5, 13).
6.      Shughulikia Sababu Za Asili
Wakati Eliya alipokuwa amechoka na kukata tamaa, Mungu alimpelekea chakula na pumziko kabla hajashughulika na sababu zenyewe na kumpa neno jipya, mwelekeo mpya, na tumaini jipya (1Fal 19:3-18).
7.      Simama Kwenye Ahadi Ya Mungu
Petro anatuasa kuwa wanyenyekevu chini ya mkono wenye nguvu wa Mungu, kumtwika Yeye fadhaa zetu, kuwa na kiasi, kumpinga Shetani na kuwasaidia wengine wanaoteseka. Anatupa tumaini kubwa kwa kusema kwamba Mungu wa neema yote atatujia mara ili kututengeneza, kututhibitisha na kututia nguvu (1Pet 5:6-11).

Comments

Popular posts from this blog

LINDA SAANA MOYO WAKO KULIKO VYOTE ULINDAVYO: JINSI YA KULINDA MOYO WAKO-I

VINYWA VYA MOYO: JINSI YA KULINDA MOYO WAKO-2

Ufanye Nini Unapoumizwa Moyo Na Watu Wako Wa Karibu/ Jinsi Ya Kupokea Uponyaji kwa Moyo Ulioumizwa