Kitabu Cha Mwongozo Wa Kuishi Mtindo Wa Maisha Ya Kikristo

 



Biblia iliandikwa kama kitabu cha Mwongozo kwa Mkristo. Kimejaa visa vingi vya watu halisi walio kama sisi waliokabiliwa na changamoto zile zile tunazokutana nazo kila siku. Kuwafahamu wahusika hao wa Biblia - furaha na huzuni zao, matatizo yao na nafasi zao nzuri walizopata hutusaidia sisi kukomaa kama Wakristo.
Mtunga Zaburi, Daudi aonyesha mfano wa kulitegemea Neno la Mungu kila siku kwa kulilinganisha na mwanga wa tochi (kurunzi);
"Neno lako ni taa ya miguu yangu na mwanga wa njia yangu." Zaburi 119:105. (Isipokuwa pale ilipoelezwa vinginevyo, mafungu yote ya Maandiko katika GUNDUA Miongozo yanatoka katika Toleo Jipya la Kimataifa la Biblia - New International Version (NIV).

Nuru tunayoipata kila siku kutoka katika Biblia inafunua wazi sifa zile tunazozihitaji katika maisha yetu na kanuni za kukua kiroho. Zaidi ya hayo yote, Biblia inatuonyesha Yesu, Nuru ya Ulimwengu. Maisha yetu yana maana tu anapoyaangazia Yesu kwa Nuru yake.

Comments

Popular posts from this blog

LINDA SAANA MOYO WAKO KULIKO VYOTE ULINDAVYO: JINSI YA KULINDA MOYO WAKO-I

VINYWA VYA MOYO: JINSI YA KULINDA MOYO WAKO-2

Ufanye Nini Unapoumizwa Moyo Na Watu Wako Wa Karibu/ Jinsi Ya Kupokea Uponyaji kwa Moyo Ulioumizwa