Kwanini Kujiinamia/ Kukata Tamaa?

 



Ujasiri huja kwa kutiwa moyo, na kinyume chake ni kuvunjika moyo na ni pale kitu fulani kinaposababisha ujasiri wetu kutoweka. Zifuatazo ni baadhi ya sababu zilizowafanya watu kwenye Biblia kuvunjika moyo. Sababu hizo ni  kama zifuatazo.
1.      Ugumu Wa Safari Yenyewe
Katika Hes 21:4 wale watu walikuwa wamechoshwa na safari ya kuelekea kwenye nchi ya ahadi. Jangwa lilikuwa linawaletea madhara.
2.      Takataka Za Zamani
Katika Neh 4:10 wale watu walikuwa wamechoka kwa kubeba kifusi na mawe ya zamani. Hilo laweza kuwa kweli hata kwetu pia ikiwa tabia za zamani zinaweza kuturudia na kutusababisha kuanguka.
3.      Maneno Kutoka Kwa Adui
Katika Neh 4:11 maadui wenyeji waliongeza wingi wa maneno ya kukatisha tamaa.
4.      Unapoacha Kumwangalia Yesu
Katika Zab 73:2,3 mwandishi anashuhudia kwamba ilikuwa nusura aanguke alipoacha kumtumaini Mungu na kuanza kutamani mafanikio ya watu waovu. Hatari!
5.      Njia Za Siri Au Zidanganyazo
Katika 2Kor 4:2 Paulo anajua jinsi inavyoweza kukatisha tamaa wakati watu wanapofanya mambo yao ya aibu kwa siri.
6.      Mungu Wa Dunia Hii
Huyo ni Shetani, aliyetajwa katika 2Kor 4:4. Mungu ndiye anayekupa saburi na faraja, Rum 15:5, ili upate kujua ni nani anayewaondolea hali ya kuvunjika moyo.
7.      Kujijengea Himaya Binafsi
Hakuleti baraka za Mungu bali hupelekea kushindwa na kuvunjika moyo (2Kor 4:5).
8.      Uchovu Na Udhaifu Wa Mwili
Katika 2Kor 4:7 Paulo anatufananisha sisi na vyombo vya udongo ili kuonesha jinsi tulivyo wepesi kuvunjika, na kwamba tunayo hazina tukufu ya Mungu ndani mwetu. Kumbuka kwamba vyombo vya udongo vina wepesi wa kuvunjika au kupata mpasuko; na vivyo hivyo miili yetu na akili zetu ikiwa tutazifanyiza kazi kupita kiasi.
9.      Shughuli Za Mungu
Kama tutasahau kwamba Mfinyanzi Mkuu sikuzote yuko katika utendaji wa kutufinyanga, kutupa sura na kutunyoosha ili tufanane zaidi na Yesu, tunaweza tukakatishwa tamaa na baadhi ya mambo yanayofanyika katika karakana ya Mungu (2Kor 4:8-11).

Comments

Popular posts from this blog

LINDA SAANA MOYO WAKO KULIKO VYOTE ULINDAVYO: JINSI YA KULINDA MOYO WAKO-I

VINYWA VYA MOYO: JINSI YA KULINDA MOYO WAKO-2

Ufanye Nini Unapoumizwa Moyo Na Watu Wako Wa Karibu/ Jinsi Ya Kupokea Uponyaji kwa Moyo Ulioumizwa