MAOMBI YA TOBA MBELE ZA MUNGU
Anza kwa kumshukuru Mungu kwa wema na fadhili zake nyingi mno kwa maisha yako na kwa ajili ya matendo yake makuu. Baada ya hapo unaweza kuingia kwenye toba kwa kutumia maandiko yafuatayo. Itakuwa vema kama utatumia Biblia yako na unaweza kusoma mistari hii huku unaomba. (Me huwa napenda kuomba huku natembea tembea, Kila mmoja ana aina yake pia)
Kut 20: 1 -4.
Zaburi 130:3
Isaya 59:1-2,
Yohana 9:31,
1Yohana 1:8-9,7
Baada ya kumaliza kutubu sasa tumia mamlaka ya Damu ya Yesu maana ndio inatupa uhalali wa kukisogelea kiti cha Enzi cha Mungu baba.
Kumbuka Yesu alipomwaga damu yake pale msalabani alilipa fidia kwa ajili ya maisha yetu ya sasa na yale yajayo. Mwambie shetani hunidai chochote maana Yesu alilipa madai yote pale msalabani.
Ufunuo 12:10. "Nikasikia sauti kuu mbinguni, ikisema, Sasa kumekuwa wokovu, na nguvu, na ufalme wa Mungu wetu, na mamlaka ya Kristo wake; kwa maana ametupwa chini mshitaki wa ndugu zetu, yeye awashitakiye mbele za Mungu wetu, mchana na usiku.".1Petro 1:8,
Kolosai 2:3-14 "akiisha kuifuta ile hati iliyoandikwa ya kutushitaki kwa hukumu zake, iliyokuwa na uadui kwetu; akaiondoa isiwepo tena, akaigongomea msalabani; akiisha kuifuta ile hati iliyoandikwa ya kutushitaki kwa hukumu zake, iliyokuwa na uadui kwetu; akaiondoa isiwepo tena, akaigongomea msalabani;"
Omba kwa Imani na piga mapepo yote yanayotunza kumbukumbu Sema Kwa jina la Yesu leo napiga watunza kumbukumbu wote, kwa jina la Yesu’ KWA JINA LA YESU KTRISTO WA NAZARETI MWANA WA MUNGU ALIYE HAI LEO NAWAPIGA NA KUWATEKETEZA WATUNZA KUMBUKUMBU ZOTE MBAYA DHIDI YA MAISHA YANGU,FAMILIA, UKOO,KWA JINA LA YESU.....YESU…..
maana kuna wengine wamefungwa toka tumboni kutokana na madhambi ya mababu na mabibi zao! Mfano bibi alikuwa mchawi, wanachofanya mapepo wanakwenda mbele za Bwana na kutoa mashtaka kuhusu familia yako. Wanamwambia kwa kuwa bibi yake alikuwa mchawi na aliwazuia wengi kuolewa na huyu haturuhusu kumzuia kuolewa, Mungu akinyamaza tayari ndo tiketi ya wao kukuvuruga. Mungu hawezi kukuadhibu ila mashetani ndo hutunza kumbukumbu na kwenda kukushtaki mbele za Bwana kwa kutumia sheria za Mungu. Ndio mana inatokea mtu yanampata mabaya wakati hakutenda kosa lolote
"Kwa jina la Yesu, nashambulia watunza kumbukumbu wote wanaotunza kumbukumbu za familia yangu na ukoo wangu toka ukoo wetu ulipoanza mpaka hapa nilipofikia mimi"
Tumia Damu ya Yesu Kufuta Hati zote za Mashtaka ambazo shetani anazitumia kila siku kukushtaki mbele za Mungu na ndio zinazozuia baadhi ya mambo yako unayoyaona yanakwama,
Zaburi 147, 148
Futa hati ya mashitaka na ondoa uhalali wa shetani kututawala na kukutumikisha, Kol.2: 14
Kuwa na Ujasiri mbale za Mungu 1 Yhn 3: 21- 22, Mwanzo 3: 8 – 19.
Baada ya hapo shukuru Mungu tena maana amekuweka huru na hati zote zimeshafutwa hakuna tena pepo mwenye kumbukumbuku anayeweza kuzia maombi yako unaweza kuchukua lile karatasi lako lenye mahitaji na malengo yote uliyojiwekea kwa mwaka huu na kuanza kuyaombea kwa kusimamia Neno kama ifuatavyo.
Wafilipi 4:6-7,19 Isaya 43:26
Yohana 16:24
Marko 11:23
Yohana 14:12-14;
Mathayo 7:8-11
Luka 11:10
Mungu Awabariki sana na kuwajalieni yote
Wapenzi naomba mfanikiwe katika mambo yote na kuwa na afy njema , kama vile roho zenu zifanikiwavyo.1 Yohana 1:2
By Mary Muna kwa Niaba ya Ndugu Mecky Kasmiry Kutokana na Simu yake imepata shida kidogo Unaweza kumkumbuka Mungu amjalie apate simu nzuri aendelee na huduma hapa..
Comments
Post a Comment