MFUNDISHE MTOTO KUOMBA KWA MUNGU
Mtoto anatakiwa afundishwe kumshukuru Mungu kwa mambo mbalimbali ya maisha yake kama vile,afya, wazazi, , chakula, nguo na mengineyo mfano kumwomba Mungu pale anapopata hofu, huzuni au kuumizwa. Ni vizuri pia ajifunze kuwaombea wadogo na wakubwa wake, walimu wake, marafiki zake na majirani pia. Hii itamjengea pia upendo kwa watu ambao anawaombea. Mweleze kuwa Mungu anampenda na anasikia maombi yake na anapenda kuzungumza naye.
Wazazi wanatakiwa kuomba na watoto wakati wa Kula, akiamka asubuhi, usiku wakati wa kulala, anapoondoka kwenda shule na pale unapomuombea mtu mwenye mahitaji umfundishe kumshukuru Mungu pale maombi yake yanapojibiwa.

Comments
Post a Comment