MFUNDISHE MTOTO WAKO KUJIAMINI

 



Mada hii ya leo  ni masda inayohusu mbinu zakumfanya  mtoto wako aweze kujiamini.Pamoja na mambo mengine hatua kadhaa zinazofaa kuchukuliwa na mzazi au mlezi katika suala kumjengea  mtoto  uwezo wa kujitambua hivyo kuwa na tabia ya kujiamini ambayo ni moja ya nyenzo muhimu kwa mtu kufikia mafanikio katika malengo aliyo jiwekea maishani.
Ni Vizuri Kumtia Moyo kwa mambo yake Unapo kusudia kumjengea mtoto tabia ya kujiamini na kujitambua na uonapo umetenda sawa na inavyotakiwa,umpe mtoto maneno mazuri  yenye kumtia moyo na kumuonesha kuwa ni mshindi
Usiache kumkosoa  anapo kosea  na kumkanya anapofanya kosa. Nijukumu lako mzazi  kutambua umuimu wako kwa mtoto na kumweleza ukweli anapokosea ukasimama kidete kuhakikisha anarejea katika mstari  kwa njia yoyote unayoamini kuwainafaa bila kumuathiri kimwili au kiakili.Muimarishe kifikra kwamba upo kwaajili ya kuakikisha anakuwa katika msingi unao kubalika.Anapokosea  hakikisha  pia unamfanya aamini kuwa hakushindwa bali ndio njia yakujifunza  kufanyakazi kwa ufasaha maana wahenga walisema watu wanajifunza kutokana na makosa ingawa si vyema kukosea hatapasipo na sababu.
Kumsifia niatua inayo faa sana katika kumjengea mtoto kujiamini .Huwezi   na wala utakiwi kuiepuka usipo msifia na kumpongeza ataisi jitiada zake hazikuzaa matunda ipasavyo.Maoni ya mzazi katika kazi yoyote inayo fanywa na mtoto
Ni jambo muimu kuliko lolote duniani.Mtu anapofahamu kuwa mzazi wake anaona na kufuatilia anachofanya na kumpa maoni iwekumkosoa na kumpongeza anapata imani kuwa anaweza. Unapo mfunza jambo pendelea kutumia mifano huku ukimwonesha namna ya kujieleza cheka naye na mtaniye ili ilikumfanya awehuru na karibu zaidi na wewe.Kicheko sio tu  kinafaa kiafya lakini unapo weza kusababisha muingie katika hali ya kicheko inafanya ajihisi vizuri.Ukimudu kumfanyia hayo naye atajifunza kutoka kwako.Kiwango hicho cha malezi kitamfunza kujiamini pamoja nakuwanauwezo wakukabiliana na matatizo hatakama akiwambali na wazazi au walezi wake.jumuika naye katika kutekeleza baadhi ya shughuli.Anapo tekeleza shughuli  kwa mara ya kwanza  na asifanikiwe kuitekeleza kwa ufasahaa na kwakiwango kinachofaa.Mweke karibu yako huku ukitekeleza naye akifuatilia unavyo tekeleza.Wakati mwingine umwache atekeleze mwenyewe iliuone kama atafanikiwa.Anapo fanikiwa usisahau kumpongeza naanapo kosea usisahau kumkosoa ukimtia moyo kuwa huo ndio mwanzo wa kufahamu.Anapokueleza kuwa kunakitu shuleni kwao kimetendeka kimakosa,mathalani anuani ya shuleni kwao imeandikwa tofauti nainavyo takiwa jipemuda kumsikiliza na kufuatilia   ilikuakikisha naunapo baini kuwa anachoamini ndicho kinachotakiwa.Hii itamjengea  uwezo katika kufanya mawasiliano,kufikiri kujiamini na jinsi yakufanya majadiliano ya kimaendeleo  ambayo hayo yote yanajikita katika tabia ya uaminifu.Hepuka tabia ya kupuuza hoja zake.Jadiliana naye napenda kushiriki michezo mbalimbali pamoja naye jambo ambalo litamfundisha nakumpa uwezo wakuona mambo katika mtazamo tofauti.Hizi ndizo funguo za kujenga mtoto au mtu tabia ya kujiamini
A.K.A.Usikubali kua yupo sahihi au amekosea bila kufanya mahojiano naye juu ya suala husika.Hii inatokana na ukweli kwamba mjadala utampa fursa ya kujifunza  nakubaini alipokosea  kirahisi hivyo umuezesha kujirekebisha na kukuza uwezo wake wa kujiamini haraka.Kua makini mfunze kuamini kua sio kweli wakati wote atakua sahihi usipo fanikiwa kumjenga katika hali hiyo utamuumbia tabia ya kujikweza jambo ambalo nitofauti na tabia ya kujiamini unayo  kusudia kumjengea.  

Comments

Popular posts from this blog

LINDA SAANA MOYO WAKO KULIKO VYOTE ULINDAVYO: JINSI YA KULINDA MOYO WAKO-I

VINYWA VYA MOYO: JINSI YA KULINDA MOYO WAKO-2

Ufanye Nini Unapoumizwa Moyo Na Watu Wako Wa Karibu/ Jinsi Ya Kupokea Uponyaji kwa Moyo Ulioumizwa