MSIFU, MUABUDU NA MSHUKURU MUNGU. Zaburi 147 na Zaburi 148

Baba yetu uliye mbinguni, jina lako litukuzwe, jina lako liinuliwe, jina lako libarikiwe; kwakuwa jina lako, lapita majina yote. Ee Mungu, hakuna Mungu mwingine aliye kama wewe. Peke yako, ndiwe Mtakatifu, peke yako, ndiwe mwaminifu sana, peke yako ndiye uliye juu. Hakuna Mungu kama wewe Baba, kwa maana, peke yako ndiye mwenye rehema na upendo mkuu namna hii, hata kuusmehe maovu yetu na kutoyakumbuka kabisa. Wewe ni Mungu mwenye upendo na rehema.

Baba, Wewe ni Mungu mwenye nguvu za ajabu, peke yako ndiye unayeweza mambo yote; hakuna lililo gumu kwako. Baba, wewe ndiwe uliyejaa hekima na nguvu. Hakika, hakuna Mungu kama wewe Bwana. Ee Mungu wa mbinguni, ninakuabudu kwa tabia zako; na ninakusifu wewe peke yako, kwasababu ya matendo yako ya ajabu. Nami ninakutukuza pia, kwa ajili ya yale uliyokusudia kufanya na kwa yale uliyoahidi kufanya katika maisha yetu Baba. Pokea sifa zangu/zetu na ibada yangu/yetu. Hakika, hakuna Mungu kama wewe. Huko mbinguni, huku duniani na hata kule kuzimu, hakuna Mungu kama wewe. Jina lako libarikiwe sana, Ooh Haleluyah! Kwasababu
Wewe ndiwe Adonai, kwa maana wewe ndiwe Mungu mwenye enzi yote, uliye juu ya yaote.
Wewe ndiwe El- Ohinu, kwa maana wewe ndiwe Bwana Mungu wetu, sina kimbilio jingine.
Wewe ndiwe El-Gibor, kwa maana wewe ndiwe Mungu mwenye nguvu zote.
Wewe ndiwe El-Eliyon,  kwa maana wewe ndiwe Mungu uliye juu sana sana.
Wewe ndiwe Elohim, kwa maana wewe ndiwe Mungu muumbaji wa hivi vitu vyote.
Wewe ndiwe Jehovah Mekadesh, kwamba wewe ni Mungu utakasaye na kutousha makosa yetu
Wewe ndiwe Jehovah Shamah, Mungu wangu unayenizunguka na kunijaza kwa uwepo wako.
Wewe ndiwe Jehovah Saboath, Mungu wangu unayenipigania kwa majeshi yako na nguvu.
Wewe ndiwe Jehovah Nisi, Mungu wangu unayenishindia vita na mapambano yangu yote.
Wewe ndiwe Jehovah Rafa, Mungu wangu unayeniponya na kuhuisha afya yangu kila siku.
Wewe ndiwe Jehovah Shalom, Mungu wangu unayenijaza kwa amani yako na furaha yako.
Wewe ndiwe Jehovah Rohi, Mungu wangu unayenichunga na kuniongoza ktk malisho mazuri.
Wewe ndiwe Jehovah Yire, Mungu wangu mtoaji, unayenipa kila kitu ninachohitaji maishani.
Wewe ndiwe El-Shaddai, Mungu wangu unayenitosheleza kwa yote ninayohitaji maishani.
Ee Baba yangu, Jina lako libarikiwe, jina lako litukuzwe, jina lako liinuliwe kuliko majina yote

Comments

Popular posts from this blog

LINDA SAANA MOYO WAKO KULIKO VYOTE ULINDAVYO: JINSI YA KULINDA MOYO WAKO-I

VINYWA VYA MOYO: JINSI YA KULINDA MOYO WAKO-2

Ufanye Nini Unapoumizwa Moyo Na Watu Wako Wa Karibu/ Jinsi Ya Kupokea Uponyaji kwa Moyo Ulioumizwa