. Mwongozo Kwa Maisha Yenye Furaha
Kitabu cha Mhubiri ni taarifa ya utafiti wa Sulemani juu ya furaha. Anaandika kumbukumbu ya safari zake za kutafuta furaha katika utajiri wa ulimwengu huu, nyumba za kifahari, mashamba ya mizabibu izaayo sana, bustani nzuri sana, na mashamba ya miti ya matunda matamu sana yenye harufu nzuri. Aliongeza idadi ya watumishi wake. Alijikuta amezungukwa na kila kitu ambacho mtu angeweza kukitamani. Lakini furaha ikateleza na kwenda mbali naye, ndipo akaandika, akasema. "Nilipozichunguza kazi zote zilizokuwa zimefanywa na mikono yangu, na kusumbuka kwangu kote katika kuzitenda, kila kitu kilikuwa hakina maana kabisa, ilikuwa ni sawa na kujilisha upepo" - (Mhubiri 2:11).
Ndipo Sulemani alipogeuka ili kuzitafuta anasa za ulimwengu huu kwa tumaini la kuipata furaha. Akatawaliwa na mvinyo, wanawake, na nyimbo. Hitimisho lake ni hili:
"Bure kabisa, bure kabisa, nakuambia mimi, Mhubiri! Kila kitu ni bure kabisa" (Mhubiri 12:8.
Zamani Sulemani alikuwa amepata kuonja na kuona ya kuwa Bwana yu mwema. Alipoyalinganisha maisha yake yale ya kwanza ya utii wake kwa Mungu na maisha yake ya kutafuta furaha katika mambo ya dhambi bila kujali kitu, wosia wake ukawa ni huu:
"Hili ndilo hitimisho la jambo hilo: Mche Mungu, na kuzishika amri zake, kwa maana huo ndio wajibu wote umpasao mtu." - Mhubiri 12:13.
Sulemani aliona angeweza kutafuta njia ya mkato ya kupata furaha kwa kuishi maisha mapotovu. Karibu na mwisho wa maisha yake, alikuwa mwanaume tosha kuweza kukiri kosa lake. Ili kuwaokoa wengine wasitende kosa lile lile, aliandika maneno haya, "Yule aitunzaye Sheria, ana furaha." Mithali 29:18, KJV.
Comments
Post a Comment