MZAZI MWELEZE MTOTO HABARI ZA MUNGU
Mzazi unatakiwa kumwonesha mtoto wako vitu vyote pamoja na uumbaji wote wa Mungu
Onesha upendo wako kwa mtoto kwa kila jambo unalofanya ukiwa naye mfano: unapomlisha, unapomwogesha au unapomwogesha mweleze kuwa yeye ni zawadi yako toka kwa Mungu na umepewa umtunze na kumlea katika maadili mema yanayompendeza Mungu pekee n asi vinginevyo..
Mwambie mwanao Mungu anampenda sana na wewe pia unampenda kwa upendo wa dhati wala hakuna mwingine atakayempenda kama wewe.
Mwambie mwanao juu ya kusudi la Mungu kwa watu wote ni kupendana, mfundishe namna ya kupendana na wenzake anapokuwa shuleni, anapocheza na chochote anachofanya kwa kushirikiana na wenzake hata kama sio ndugu zake wa kuzaliwa naye awapende.
Mtoto wako anapokosea mweleze juu ya maagizo ya Mungu na amri zake na kuwa imempasa kuyashika na kutotenda kinyume na maagizo hayo ya Mungu..
Mfundishe na kumweweleza kuhusu ulinzi wa Mungu unapompeleka kulala na anapokwenda shule.

Comments
Post a Comment