Neema Ya Mungu Na Utii Wetu Kwa Sheria Yake
Wokovu ni zawadi. Hatuwezi kuufanyia kazi ili tuweze kustahili kuupata. Tunaweza tu kuupokea kwa imani. Tunakupokea huko kuhesabiwa haki (kuwa katika msimamo sahihi na Mungu) kama zawadi; kwa njia ya imani peke yake kwa sababu ya neema yake Mungu.
"Kwa maana MMEOKOLEWA KWA NEEMA, kwa njia ya IMANI-na hiyo haitokani na nafsi zenu wenyewe, ni ZAWADI TOKA KWA MUNGU - Si kwa matendo, mtu yeyote asije akajisifu" Waefeso 2:8.
Hatuwezi kuzishika amri hizo kwa matendo yetu wenyewe - yaani, kwa kujitahidi kwetu. Hatuwezi kuzishika amri hizo ili tupate kuokolewa. Lakini tunapomwendea Yesu kwa imani na unyenyekevu na kuokolewa naye, hapo ndipo upendo wake unaijaza mioyo yetu. Kama matokeo ya neema hiyo ya Mungu na kukubaliwa naye, sisi tunaingiwa na shauku ya kumfuata yeye na kumtii kwa njia ya uwezo wa upendo wake ulio ndani ya mioyo yetu (Warumi 5:5).
Paulo anatilia mkazo wake juu ya kutokufaa kabisa kwa juhudi za kibinadamu, naye anadokeza kwamba sisi hatuko chini ya sheria kama njia ya kujipatia wokovu wetu, bali tuko "Chini ya neema."
"Je! Tutende dhambi (tuzivunje Amri kumi) kwa sababu hatuko chini ya sheria (amri kumi) bali chini ya neema? Hasha!" - (Warumi 6:15).
Kwa nini? Kwa sababu moyo ule unaosukumwa na upendo unazaa maisha ya utii utokanao na upendo huo! (Warumi 13:10). Kumpenda Kristo ni kumtii yeye.
"Yeye aliye na amri (kumi) zangu na kuzitii, ndiye anipendaye mimi." Yohana 14:21.
Eric Liddel alidhihirisha kwamba, hata katika mazingira mabaya sana, muumini aliyepewa uweza wa Mungu unaweza kuishi maisha ya kuridhika, maisha ya utii. Liddell alionyesha wazi tabia yake iliyowavutia watu katika kipindi kile cha dhiki na hofu. Uhusiano wake wa upendo kwa Kristo ulimtia nguvu kwa njia ya Roho Mtakatifu, na kumwezesha kuyatimiza "matakwa ya haki yanayodaiwa na sheria" (Warumi 8:1-4). Uhusiano wa upendo na yule Mwokozi aliyesubiliwa na kufufuka unaweza kuzaa aina hiyo ya maisha.
Je! Hivi wewe umeigundua mwenyewe siri hii? Upendo wa Kristo kwa ajili yako ulimfanya atoe maisha yake kwa ajili ya dhambi yako. Yeye anajitolea kuutia nguvu uhusiano wako wote kwa kukupa upendo wake na kuku "fan(ya) (wewe) kuwa (m) kamilifu katika kila tendo jema ili upate kutenda mapenzi yake" (Waebrania 13:12). Jibu lako ni lipi?
Comments
Post a Comment