NIfanyeje niwe na furaha?

 



Mwaka 1943, majeshi ya Uvamizi ya Kijapani yaliwaamuru wale "Wananchi Maadui" wa Kimarekani na Ulaya kwenda katika kambi la waliotekwa vitani katika lile Jimbo la china la Shantung.
Walilazimika kustahimili miezi mingi ya kuchosha sana, ya kukata tamaa, ya kusongamana pamoja na ya hofu. Watu wenye tabia tofauti waligongana, hasira zililipuka. Magomvi madogo madogo yaliongezeka sana.
Lakini mtu mmoja alielezwa na mfungwa mmoja wa kivita kwamba "bila shaka lolote alikuwa ni mtu aliyehitajika sana na kuheshimiwa sana, tena aliyependwa sana katika kambi lile. "-Eric Liddell, Mmishonari kutoka katika nchi ya Waskoti (Scotland).
Malaya mmoja wa Kirusi katika kambi lile baadaye aliweza kukumbuka ya kwamba yule Liddell ni mwanaume peke yake aliyeweza kumtendea yule mwanamke jambo lolote bila kutaka kulipwa kimwili. Mwanamke yule alipokuja mle kambini kwa mara yake ya kwanza, akiwa peke yake, na mwenye kudharauliwa, ndiye aliyemtengenezea yeye baadhi ya rafu za kuwekea vitu vyake.
Mfungwa wa vita mwingine alikumbuka kwamba, "yeye alikuwa na mbinu ya upole, na ya kuchekesha iliyozilainisha hasira zao zilizovurugika vibaya".
Katika mkutano mmoja uliojaa hasira wa wafungwa wale wa kivita, kila mmoja alikuwa akitoa madai yake kwamba mtu fulani mwingine ndiye angefanya kitu fulani kwa wale vijana watukutu wenye umri wa kuanzia miaka kumi na mitatu hadi kumi na tisa (matineja) ambao walikuwa wanajitia katika matatizo. Liddell akatoa suluhisho lake. Aliandaa michezo ya kujiburudisha, ufundi wa kutengeneza vitu kwa mikono, na madarasa kwa ajili ya watoto wale, na kuanza kutumia wakati wake wa jioni pamoja nao.
Liddell alijipatia sifa na utukufu katika Michezo ya Olimpiki ya mwaka wa 192, alijinyakulia nishani ya dhahabu katika mbio za mita 400. Lakini katika uwanja ule mdogo sana wa kambi lile alijionyesha pia ya kuwa ni mshindi katika zile mbio za Kikristo, akajipatia sifa kutoka kwa wafungwa wa vita wale walioipenda sana dunia hii.
Je! Ni kitu gani kilichomfanya kuwa mtu wa aina yake? Ungeweza kuwa umeigundua siri yake saa 12 kila asubuhi. Ule ndio wakati alipotoka kimya kimya kwa kunyatia akiwapita wenzake waliolala usingizi, na kutulia kimya mezani, na kuiwasha taa ndogo ili itoe mwanga wa kumwezesha kuliona daftari lake ndogo na Biblia yake. Eric Liddell alitafuta neema na nguvu kila siku kutoka katika utajiri wa Neno la Mungu.

Comments

Popular posts from this blog

LINDA SAANA MOYO WAKO KULIKO VYOTE ULINDAVYO: JINSI YA KULINDA MOYO WAKO-I

VINYWA VYA MOYO: JINSI YA KULINDA MOYO WAKO-2

Ufanye Nini Unapoumizwa Moyo Na Watu Wako Wa Karibu/ Jinsi Ya Kupokea Uponyaji kwa Moyo Ulioumizwa