SABABU ZA KUWAFUNDISHA WATOTO NENO LA MUNGU


 Sababu Za Kuwafundisha Watoto Neno La Mungu
(a)        Watoto wanatakiwa wafahamu neno la Mungu na Mungu mwenyewe wakiwa wadogo
(b)        Watoto wanatakiwa kuwezeshwa kumtii Yesu Kristo na neno lake
(c)        Watoto wanatakiwa wajue kumwabudu Mungu katika Roho na Kweli
(d)       Watoto  wanaomjua Kristo wanaweza kubadili Taifa/dunia ya kesho
(e)        Watoto wanatayarishwa wawe watoto hai  na kuwa  viongozi  wa kesho wanaongoza Kanisa katika njia sahihi
(f)        Wawe  viongozi wa kesho wanaongoza Taifa  katika njia sahihi na hofu ya Mungu

Wazazi  wetu wana hamu  kubwa sana ya kuona watoto wao wanabarikiwa  na kukua katika misingi ya Neno la Bwana. Ni wajibu wa mzazi Mkristo kuwafundisha watoto wakiwa bado na umri mdogo na hata atakapokuwa hataacha njia ya BWANA. Haya yote ni kwa ajili ya kutimiza maagizo ya Yesu ya aliyosema 

Ni wajibu wetu kuwafundisha watoto namna Mungu anavyofanya kazi kwenye maisha ya watu wengine, ili waweze kujifunza na kuona kweli Mungu anaweza kubadilisha maisha ya watu na inawezekana kabisa kuishi maisha ya kumpendeza Mungu. Pia, tuwatie moyo katika maisha yao ya kiroho kila siku ili waweze kusonga mbele katika maisha yao.

Comments

Popular posts from this blog

LINDA SAANA MOYO WAKO KULIKO VYOTE ULINDAVYO: JINSI YA KULINDA MOYO WAKO-I

VINYWA VYA MOYO: JINSI YA KULINDA MOYO WAKO-2

Ufanye Nini Unapoumizwa Moyo Na Watu Wako Wa Karibu/ Jinsi Ya Kupokea Uponyaji kwa Moyo Ulioumizwa