Sifa Na Ibada Kwa Mungu
Zaburi 22:3
Wewe U Mtakatifu, nawe “UNAKETI” juu ya sifa za Israel
Zab 22:3
IDABA ndio kitu cha kwanza kabisa katika moyo wa Mungu, kwa sababu
MUNGU ANAISHI KATIKA IBADA na SIFA.
Kumnyima Mungu ibada Ni kama kumnyima
• Samaki maji
• Mimea udongo
• Binadamu hewa
Kwa maana, Baba anawatafuta watu wa aina hiyo ili wamwabudu.” (Yohana 4: 23),Ufunuo 4:9-11, Ufunuo 5:11-14
Mungu anatamani sana kukaa na sisi watoto wake hapa duniani, ndio maana anataka dunia yote ijazwe hali ya ibada (atmosphere) kama ilivyo mbinguni (masaa 24), ili duniani pia, kuwe na mazingira ya maisha au ya makazi ya Mungu kama ilivyo mbinguni.
Ibada nzuri hutoka katika moyo uliotulia na pia maisha mazuri; na maisha mazuri huchangiwa sana na mazingira mazuri. Kumbukumbu 8:6-18
Mazingira yakitibuka, maisha yanatibuka, na maisha yakitibuka, ibada kwa Mungu pia inatibuka.
Kutokana na umuhimu na unyeti wa ibada, Mungu hakutaka na hataki watoto wake, tuwe na maisha ya taabu, maisha ya dhiki na maisha ya shida
Comments
Post a Comment