UMUHIMU WA KUFUNDISHA WATOTO NENO LA MUNGU

 

“Basi wakamletea watoto wadogo ili awaguse; wanafunzi wake wakawakemea. Ila Yesu alipoona alichukizwa sana, akawaambia, waacheni watoto wadogo waje kwangu, msiwazuie kwa maana watoto kama hawa ufalme wa Mungu ni wao” (Marko 10:13 -16)
Ili kulitimiza agizo la Bwana Yesu katika kuwafanya watu kuwa wanafunzi wa Yesu  imetupasa kuangalia pia huduma kwa watoto wetu maana wengi wamewasahau watoto kwamba nao wanahitaji neno la Mungu. (Mathayo 28:19-20 ) Hivyo ni jambo la muhimu kuwafundisha watoto kumjua Bwana wetu Yesu Kristo na kuokoka maana watoto pia wanahitaji kuokoka. ( Unaweza kujiuliza watoto wanaokokaje wakati wamezaliwa kwenye familia ya wacha Mungu)  Watoto wengi huenda tu kanisani kwa sababu ya wazazi wao na ndani ya mioyo yao hawajampokea Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yao.
Watoto hujifunza kusifu, kuabudu, kuomba na pia hufundishwa neno la Mungu. Haya yote yanatakiwa kufanywa katika muda ambao wazazi wao wanakuwa katika kujifunza pia.
Katika Biblia tunasoma mistari mbalimbali inayotuonesha umuhimu wa kuwafundisha   watoto Neno la Mungu

1.      Watoto ni wajumbe wa habari njema ya Neno la Mungu, Yoeli 1:3 “Waarifuni watoto wenu habari yake ,Watoto wenu wakawaambie watoto wao, Na watoto wao wakakiambie kizazi kingine”

2.   Bwana anahitaji kuwaokoa, Yohana 3:16 “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele 

3.   Watoto wanaofundishwa  Neno la Mungu  mapema ni rahisi kuelewa na kukua kwa maadili ya msingi wa neon la Mungu uliowajengea.  Mithali 22:6 “ Mlee mtoto katika njia impasayo,Naye hataicha hata atakapokuwa mzee 

4.      Watoto na watu wazima/wazee wana akili tofauti, ( tunaposema wana akili tofauti ni kwamba wao wana uelewa wa kitoto na ndio maana tunaona kwamba tuna madarasa ya watoto ili kuwafundisha neon la Mungu kutokana na ufahamu wao.) 1korintho 14:20 “ Ndugu zangu, msiwe watoto katika akili zenu;lakini katika uovu mgeuzwe watoto wachanga,bali katika akili zenu mkawe watu wazima”

5.      Mwanzo wa mafanikio ya maisha yao ni nyumbani kwa wazazi wao. Waefeso 6:1-4 “ Enyi watoto,watiini wazazi wenu katika Bwana,maana hii ndiyo haki.Waheshimu baba yako na mama yako;amri hii ndiyo amri ya kwanza yenye ahadi,upate heri,ukae siku nyingi katika dunia.Nanyi,akina baba,msiwachokoze watoto wenu;bali waleeni katika adabu na maonyo ya Bwana ”

6.      Watoto ni marafiki wa Mungu, Mathayo 18:14 “ Vivyo hivyo haipendezi mbele za Baba yenu aliye mbinguni kwamba mmoja wa wadogo hawa apotee

7.      Watoto wataingia mbinguniZekaria 8:5 “Na hizo njia za mji zitajaa wavulana, na wasichana, wakicheza katika njia zake ”
Inasilitisha sana kuona baadhi ya wazazi wako busy na mambo yao wamewasahau watoto wao na kuwaachia wafanyakazi wa nyumbani, wewe kama mzazi wa kesho unatakiwa kuwa na maandalizi mazuri ya malezi ya watoto wako, hata kama upo busy kiasi gani, tafuta nusu saa kila siku ongea na wanao, waulize habari za maisha yao ya kiroho, shuleni, tafuta kufahamu hata marafiki zao huko shuleni ni wa aina gani.

Comments

Popular posts from this blog

LINDA SAANA MOYO WAKO KULIKO VYOTE ULINDAVYO: JINSI YA KULINDA MOYO WAKO-I

VINYWA VYA MOYO: JINSI YA KULINDA MOYO WAKO-2

Ufanye Nini Unapoumizwa Moyo Na Watu Wako Wa Karibu/ Jinsi Ya Kupokea Uponyaji kwa Moyo Ulioumizwa