Urafiki Unaotubadilisha Kabisa
Kristo anataka Biblia kwako iwe kama barua uliyoandikiwa mwenyewe itokayo kwa rafiki yako wa karibu sana.
"Ninyi nimewaita rafiki, kwa sababu kila kitu nilichokisikia kwa Baba nimewajulisheni." - Yohana 15:15.
Yesu anatutakia mema matupu. Neno lake linatuingiza sisi katika familia ile ya ndani ya Mungu; Yaani, ya wale anaowaambia siri zake na kuwafundisha yeye mwenyewe.
"Nimewaambieni ninyi mambo hayo, ili ndani yangu ninyi mweze kuwa na amani." - Yohana 16:33.
Ili kuweza kuionja amani hiyo, na uhusiano huo thabiti pamoja na Kristo, ni lazima tuzisome barua zake anazotutumia. Hivyo ndivyo Biblia ilivyo: ni barua zitokazo mbinguni. Usiziache barua hizo bila kuzifungua. Ujumbe uwezao kuyabadilisha kabisa maisha yako ambao unauhitaji umo ndani ya Neno hilo.
Hapa upo ushuhuda mmoja kamili uhusuo matokeo ya kuisoma Biblia. "Mimi nilihitaji msaada, nao niliupata ndani ya Yesu. Kila haja yangu ilitimizwa, njaa ya nafsi yangu ilishibishwa; kwangu Biblia ni ufunuo wake Kristo. Namwamini Yesu kwa sababu yeye kwangu ni Mwokozi wa Kimbingu. Naiamini Biblia kwa sababu nimeiona kuwa ni sauti ya Mungu rohoni mwangu. " - The Ministry of Healing, uk. 461
Comments
Post a Comment