Utii Kwa Amri Kumi Utokanao Na Upendo
Yesu anatuambia kwamba utii ni matokeo ya upendo.
"Mkinipenda, mtazishika amri zangu" - Yohana 14:15.
Tukimpenda Mungu, tutazitii amri zile nne za kwanza zinazofafanua uhusiano wetu na Mungu; na kama tukiwapenda watu, basi, tutazitii zile sita za mwisho ambazo hufafanua uhusiano wetu na wengine.
Mtu awaye yote anayezikanyaga Amri Kumi chini ya miguu yake anatenda dhambi.
"Kila mmoja atendaye dhambi anaivunja sheria (Amri Kumi); ukweli ni kwamba, dhambi ni uvunjaji wa sheria (Amri kumi)," 1Yohana 3:4.
Lakini Mungu na ashukuriwe, tunaye Mwokozi aliyekuja katika dunia hii na kufa, alifufuliwa, na sasa yu hai kwa ajili ya kusudi moja tu:
"Lakini ninyi mnajua ya kwamba alikuja ILI AZIONDOE DHAMBI ZETU."- Fungu la 5.
Ndani yetu hatuna uwezo wowote kutuwezesha kuishika hiyo sheria ya Mungu (amri kumi). Upendo wa Mungu "uliomwagwa…. Ndani ya mioyo yetu" ndilo tumaini letu la pekee
Comments
Post a Comment