Uwezo Wa Kutii
Biblia pamoja na zile Amri Kumi ni mwongozo usiobadilika, wa muhimu sana, na mkamilifu uletao maisha yenye furaha. Lakini, basi, mioyo ya watu bado inayo mapambano ndani yake. Mwanamke mmoja alijieleza kama ifuatavyo: "Mimi naamini kwamba hizo Amri kumi zinawafunga watu wote, nina hakika kwamba kuzishika huleta furaha. Nimejitahidi kwa nguvu zangu zote kuzishika, lakini siwezi kuzishika. Ninaanza kuamini kwamba hakuna mtu mwingine awaye yote anayeweza kuzishika."
Mwelekeo wa asili wa mtu ni kujaribu kuishi maisha hayo ya utii kwa hizo amri za Mungu. Lakini kujitahidi kama huko, tena na tena, kunakotoka katika moyo wenye dhambi wa mtuhuleta jibu hili la kukatisha tamaa, "Mimi siwezi kutii!" kwa nini? Kwa sababu.
"Nia yenye dhambi ina uadui na Mungu. Haitii sheria ya Mungu, wala haiwezi kuitii." Warumi 8:7.
Je! Kusudi la sheria hiyo ya Amri kumi ni nini?
"Kwa njia ya sheria (Amri kumi) sisi tunaitambua dhambi." Warumi 3:20.
Kazi ya sheria (Amri Kumi) ni kutufanya tutambue kabisa kwamba sisi" tu wenye dhambi tuliopotea na kuwa bila tumaini, ambao tunamhitaji Mwokozi.
"Sheria (Amri kumi na Sheria ya Kafara) ilipewa madaraka juu yetu kutuongoza kwa Kristo ili tupate kuhesabiwa haki kwa imani." - Wagalatia 3:24.
Yesu ndiye jibu! Mara tu sisi tunapokuwa miguuuni pake Yesu, tukiwa hatuna uwezo wowote kabisa, tunaweza kupokea msamaha kwa ajili ya dhambi zetu, pamoja na uwezo toka kwake utakaotuwezesha kuzitii amri zake kwa njia ya imani.
Comments
Post a Comment